Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Jawad Marwi, ambaye ni Katibu wa Pili wa Baraza Kuu la Hawza za Kielimu, mwanzoni mwa darsa yake ya juu ya fiqhi, alilaani msimamo wa Serikali ya Jamhuri ya Azerbaijan dhidi ya itikadi na hukumu za Uislamu pamoja na madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.). Aidha, aliwashauri viongozi wa nchi hiyo kujifunza kutokana na uzoefu wa miaka 70 ya utawala wa Kikomunisti nchini humo.
Aliongeza kuwa katika kipindi cha Muungano wa Jamhuri za Kisovieti za Kisoshalisti (USSR), kulifanyika propaganda nyingi na juhudi mbalimbali, ambapo hata kwa kuwaua wanazuoni wa kidini, walitaka kuwatenganisha wananchi hawa na Uislamu pamoja na Imam Hussein (a.s.). Hata hivyo, hawakufanikiwa katika juhudi hizo. Alieleza kuwa baadhi ya wataalamu wa mambo ya Mashariki wameonesha mshangao kuhusu jambo hilo katika ripoti zao.
Mwanachama wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza akizungumzia suala hilo, alihoji: Kwa nini viongozi wa nchi hii hawajifunzi kutokana na miaka 70 ya utawala uliokuwa ukimkana Mungu na kushindwa kwa watawala huo kuwatenganisha wananchi na Uislamu pamoja na mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s.)?
Mwalimu wa Hawza ya Qum alisema kuwa; chanzo cha mienendo hiyo ya watawala wa Azerbaijan ni fikra za Kimagharibi na Kizayuni, ambazo mwisho wake hautakuwa tofauti na njia ileile ya Ukomunisti iliyowahi kufuatwa nchini humo.
Maoni yako